Michezo

Mwaka mmoja baada ya kupigwa risasi kwa golikipa wa Afrika Kusini, huyu ni staa mwingine aliyeuwawa kwa risasi …

on

Mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Olimpia na Rangers ya Scotland ameuwawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa katika Parking za magari jijini La Ceiba Honduras, Arnold Peralta alikuwa likizo nyumbani kwao Honduras.

Kifo cha Arnold Peralta ambaye anamudu kucheza nafasi ya kiungo kwa ufasaha kinachunguzwa na maafisa usalama wa nchi hiyo, ila taarifa za awali zinaonesha kuwa Arnold Peralta alipigwa risasi sio na majambazi ila inasadikika ni watu wenye visasi lakini tukio bado linachunguzwa.

Olympics+Day+2+Men+Football+Spain+v+Honduras+ENz_YKSG4G9l

Headlines za kifo cha Arnold Peralta kupigwa risasi zinakuja ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka auwawe kwa risasi golikipa wa timu ya taifa ya Afrika Kusini na klabu ya Orlando Pirates Senzo Meyiwa, ambaye nae alipigwa risasi na majambazi ambao walienda kufanya uharifu katika nyumba ya mpenzi wake.

TL_1081310-602x400

Senzo Meyiwa

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments