Bunge nchini Peru limemteua Francisco Sagasti kuwa Rais wa Mpito, akiwa wa tatu kuiongoza Taifa hilo chini ya siku 7, anatoka Chama pekee kilichopinga kuondolewa madarakani kwa Rais Martin Vizcarra kufuatia tuhuma za ufisadi.
Sagasti (76) anashikilia wadhifa huo baada ya aliyekuwa Rais wa Mpito Manuel Merino kujiuzulu siku 5 baada ya kuteuliwa, kufuatia vifo vya watu wawili katika maandamano ya kupinga Uongozi wake.
Peru imeingia katika mvutano wa kisiasa baada ya maelfu ya watu kuandamana kupinga uamuzi wa Bunge kumuondoa Rais Vizcarra (57) madarakani wakidai Muhimili huo wa Serikali ulipanga kumpindua.
MAGUFULI ‘AMCHANA’ KABUDI “WEWE HUWEZI KUWA RAIS, INAUMWA LAKINI NAWAAMBIA UKWELI NA LUKUVI”