Vituko/ Comedy

Cheki na hii, Christmas ya Peru sio sherehe, ni kupigana ngumi mwanzo mwisho… (+Video)

on

Kila watu wana utamaduni wao, kama utamaduni wako ni kusherehekea kwa kukaa na familia yako nyumbani, basi kwingine sio hivyo… na kama umezoea kukutana na sherehe za marafiki na ndugu, basi Peru kuna sherehe za maadui !!

Countdown ya siku kuelekea Christmas inazidi kujivuta, zimebaki kama siku tatu tu hivi kuifikia December 25 2015, siku ambayo watu wengi wanasherehekea sikukuu hiyo Duniani, japo utaratibu wa kawaida uliozoeleka ni watu kufurahia kwenye siku hiyo, Peru mambo yako tofauti kidogo.

Unaambiwa utamaduni au utaratibu wa watu kusherehekea Christmas kwa maadui au watu wenye ugomvi kupigana ulianza kama njia ya kusuluhisha ugomvi kati ya watu miaka ya nyuma eneo moja linaitwa Santo Tomas hukohuko Peru, baadae ukasambaa sehemu kubwa sana…utaratibu wao uko hivi; kinaandaliwa kitu kinaitwa ‘Takanacuy– Christmas Fighting Festival

FIGHTS II

Hapo kwenye hilo tamasha, Christmas inasherehekewa kwa watu ambao wamekuwa na ugomvi siku za nyuma, wanakutana na wanapigana kwelikweli… mbali ya kupigana kunakuwa na burudani ya kudance pamoja na watu kuenjoy vinywaji mbalimbali kwenye tamasha hilo.

Unaambiwa mshindi anakuwa yule atakayeweza kumdondosha mwenzake chini, pambano likiisha na ugomvi wenu umeishia hapohapo.

Hii ni video fupi ya tamasha lenyewe mwaka 2013.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments