Habari za Mastaa

Peter Okoye wa P Square aweka wino wa kuwa balozi wa kampuni nyingine kubwa duniani!

on

Mmoja ya wasanii wanaounda kundi maarufu la P Square kutoka Nigeria, Peter Okoye anaziandika headlines baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa staa huyo wa muziki Africa amedondosha wino kuwa balozi mpya wa kampuni ya viatu ya Adidas.

OKOYE4

Peter Okoye kutoka kwenye kundi la muziki la P Square.

Ukichukuwa time na kutembelea social networks za Peter Okoye yani Twitter na Instagram utakutana na post mbalimbali zinazothibitisha dili hilo… ukitembelea page ya Twitter msanii huyo utakutana na tweet moja aliyoshare na mashabiki wake ikisema…

>>> Signed and Sealed. Meet your latest Adidas ambassador moi… And I’ve got Good news! Stay on this page<<< @Peter Okoye.

OKOYEPeter pia alichukuwa time na kushare good news hiyo na mashabiki wake wa Instagram kwa kupost picha na caption hiyo hiyo kwenye page yake…

OKOYE2

Mbali na kuwa balozi wa Adidas, Peter Okoye pia ni balozi wa kampuni ya maziwa Nigeria yenye jina ‘Olympic Milk’ na pia staa huyo wa muziki mwenye kipaji kikubwa cha kucheza ameanzisha kipindi chake cha kusaka vipaji kiitwacho ‘Dance with Peter’ ambacho kutokana na idadi kubwa ya watazamaji kuongezeka, kipindi hicho kimepata nafasi ya kuonekana kwenye vituo vikubwa, zaidi ya vitano ikiwemo Africa Magic  na MTV Base.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

 

Soma na hizi

Tupia Comments