Michezo

Wenger amaliza kazi kwa Petr Cech!! mkataba wake mpya uko hapa..

on

ch

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekamilisha mpango wake wa muda mrefu wa kunasa saini ya kipa wa Petr Cech, na sasa atautumikia klabu hiyo kwa miaka minne.

Arsenal imetoa kiasi cha Pauni milioni 10 kwa Chelsea ili kuweza kumnunua mlindamlango huyo hodari wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Czech na atakua akilipwa kiasi cha Pauni 100,000 kwa wiki.

Petr Cech mwenye miaka 33 amecheza zaidi ya mechi 400 katika misimu 11 akiwa na timu ya Chelsea na msimu uliopita aliweza kucheza mechi saba tu baada ya nafasi yake kuchukuliwa na kipa kutoka Ubelgiji, Thibaut Courtois.

Cech, alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Rennes ya Ufaransa Julai 2004 na kushinda makombe 13 akiwa na Chelsea likiwemo kombe moja la klabu bingwa na mataji manne ya ubingwa wa ligi kuu ya England.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie

 

Tupia Comments