Ligi kuu ya England inakaribia ukingoni, na tayari timu mbalimbali zimeshapata taswira kamili ya nini zimepanda kwa msimu mzima wa ligi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa.
Chelsea bado ina matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo na wiki ijayo inaweza kutangaza ubingwa endapo itaifunga Crystal Palace baada ya jana kutoka sare ya 0-0 na vibonde wa Arsenal.. Mpaka sasa Chelsea ndiyo inayoongoza kwenye msimamo wa ligi ikiwa na jumla ya pointi zake 77 mkononi.
Stori ambayo ipo kwenye headlines kwa sasa ni kuhusu kiungo wa Chelsea, Eden Hazard ambaye amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na chama cha wachezaji wa kulipwa England, PFA.
Mchezaji huyo nyota raia wa Ubelgiji ameifungia Chelsea jumla ya mabao 18 akiiwezesha kutwaa taji la kombe la ligi maarufu Capital One pamoja na kuwa mmoja ya wapambanaji waliosukuma jahazi la Chelsea kuelekea kwenye jukwaa la ubingwa kwa mara nyingine tangu mwaka 2010.
Hazard amekabidhiwa zawadi hiyo katika hotel ya Grosvenor Hotel iliyopo London.
Kwa upande wa mwanasoka bora chipukizi mshambuliaji hatari wa Spurs, Harry Kane alifanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kuwapiku kipa David De Gea wa Man United na Raheem Sterling wa Liverpool.
Tuzo ya heshima ilikwenda na Steven Gerrard na Frank Lampard kutokana na mchango wao mkubwa kwenye ligi kuu ya England.
Baada ya Hazard kutangazwa mshindi, staa wa soka Allan Shearer amesema ubora wa Hazard anafaa kuwa mchezaji bora wa dunia.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook