AyoTV

VIDEO: Alichokizungumza producer P Funk kuhusu Bongolos na ujio wake mpya

By

on

P Funk ‘Majani’ ni moja kati ya watu wenye mchango mkubwa sana kwenye muziki wa Bongofleva akiwa kati ya producers wa mwanzo kabisa kwenye muziki huu ambao wametoa mchango mkubwa.

Ayo TV na millardayo.com ilipiga stori na producer huyo ambaye hajatengeneza muziki kwa muda mrefu lakini sasa ametangaza ujio wake mpya ambapo pia ameelezea juu ya ujio wa kundi lake mpya la muziki linaloitwa Bongolos.

Kwenye video hapa chini ni siku ambayo walikuwa wanafanya video shoot ya wimbo wa kundi la Bongolos…>>>”Tunafanya shooting yetu ya vijana wangu wanaitwa Bongolos. Wasanii chipukizi, ndio ule ujio wa Majani. Mwenye muziki wake karudi ndio kitu chenyewe hiki hapa.

P Funk pia amejibu swali aliloulizwa juu ya uamuzi wake wa kurudi wakati huu na kusema…

>>>”Mimi bado ni kijana. Watu wengi wanajua mimi makamo yangu ni sawa na Master Jay. Master Jay kanizidi miaka kumi, watu hawaelewi hilo. Watu wengi wanaandika comment, wewe ungestaafu kama Master Jay, lakini mimi bado nina nafasi na ninapoenda kwenye safari yangu nazidi kujifunza.” – P Funk Majani.

Video: Baada ya P Funk kuona video ya mapenzi wanayosema ni mtoto wake >>>

Soma na hizi

Tupia Comments