Top Stories

Mwanaume afikishwa polisi kwa kujaribu kujiua baada ya kuachwa na mkewe

on

Mwanaume mmoja nchini Kenya, anashikiliwa na polisi kwa kosa la kujaribu kujiua baada ya mgogoro uliotokea baina yake na mke wake na mkewe huyo kuamua kumuacha.

Askari Polisi wa kituo cha Migori, Gladys Rutere ameeleza kuwa mtuhumiwa, ambaye jina lake bado halijawekwa wazi kwa sababu za upelelezi alipelekwa polisi hapo na waendesha bodaboda.

Inaelezwa kuwa waendesha bodaboda hao walimkuta mwanaume huyo akijaribu kuruka kwenye daraja la mto Migori na hivyo kufanikiwa kumwokoa na baadae kumpeleka polisi.

Onyo alilotoa January Makamba kwa Mastaa wa Bongo

Soma na hizi

Tupia Comments