Top Stories

Wasudan waishio Marekani waandamana hadi ikulu ya Trump….kisa?

on

Wasudan Kusini ambao wanaishi Washington DC nchini Marekani jana April 16, 2018 wameandamana hadi Ikulu ya nchi hiyo wakipinga kuendelea kwa vita nchini kwao.

Takribani waandamanaji 25 wakiwemo wa chama cha upinzani cha SPLM-IO walisikika wakipiga kelele na kusema “watu wa Sudan Kusini wanakufa na “tunahitaji amani nchini Sudan Kusini”.

Kupitia chombo cha habari nchini Marekani cha Voice of America, waandamanaji hao walishika mabango na kuvaa mashati yaliyoandikwa “Rais Trump ataifanya Sudan Kusini iwe nzuri tena.

Mabango mengine yalilenga biashara ya Afrika, Mamlaka ya Maendeleo ya Kikanda-IGAD bango lililosomeka “IGAD imeshindwa na imejaa rushwa kiasi cha kushindwa kuleta amani Sudan Kusini”.

‘Kwanini Zanzibar wamekuwa kati ya viwanja bora vya ndege, nyie hakuna’-Waziri Mbarawa

 

Soma na hizi

Tupia Comments