Habari za Mastaa

Pichaz za mastaa watano duniani wanaomiliki gari la kifahari analotaka kununua Diamond Platnumz 2016

on

Siku zinazidi kusogea toka mwaka 2016 uingie, robo ya mwaka tumeshaimaliza ila February 1 2016 msanii Diamond Platnumz akiwa katika exclusive interview na Millard Ayo alithibitisha  kuwa mwaka 2016 atanunua gari la kifahari aina ya Rolls Royce. Kwa kawaida Rolls Royce thamani yake hufikia milioni  500 za kitanzania.

Platnumz alimwambia Millard Ayo >>> ‘Nataka nibadilishe aina ya gari sababu imekua ni muda mrefu, nafikiri ni muda wa kuwa na gari nililokua nalitamani siku zote, gari la ndoto yangu ni Rolls royce na ndio ninalotaka kulinunua mwaka huu wa 2016 na litakua na jina la PLATNUMZ na sio namba za kawaida’

Kutokana na kuwa na bei kubwa Rolls Royce sio gari ambazo hutumiwa na watu wengi, March 29 nimekusogezea list ya baadhi ya mastaa watano duniani ambao wanamiliki Rolls Royce.

1- Koffi Olomide huyu ni nguli wa muziki wa dansi kutokea Kongo, inaripotiwa alinunua Rolls Royce Phantom V12 6.7 mwaka 2013 kama zawada kwa mkewe ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 20.

264517_643109372371271_1893476095_n (1)

Koffi Olomide

2- Kim Kardashian na Kanye West wapo kwenye hii list kwa kumiliki Rolls Royce yao yenye rangi nyeusi.

kIM KARDASHIAN

Kim Kardashian na Kanye West

3- Jay Z na Beyonce wapo katika list ya mastaa wa dunia wanaotembelea Rolls RoyceJay Z na Beyonce wanatumia Rolls Royce Convertible.

Jay-Z and Beyonce own a vintage Rolls Royce convertible.

Beyonce

4- Emmanuel Adebayor ambae anaeichezea Crystal Palace ya Uingereza yupo katika list ya baadhi ya mastaa wanaotembelea Rolls Royce, yeye kaiwekea namba zake binafsi za usajili yaani SEA maana yake Sheyi Emmanuel Adebayor.

Adebayor-Phantom-2wvdu9xf7ckroaqgsz79qi

Emmanuel Adebayor

5- Justine Bieber ameingia kwenye list hii kutokana na kumiliki Vintage Rolls Royce 

justine bieber vintage Rolls Royce

Justine Bieber

Hii ni video ya maelekezo ya uzuri na ubora wa Rolls Royce

Kama uliikosa interview ya Diamond Platnumz akizungumzia wanaosema Tiffah sio mtoto wake

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments