Millardayo.com imekusogezea picha 11 za tukio lililofanyika jana la Kongamano la kumbukizi ya hayati Mkapa ambapo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dr Hussein Mwinyi, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi mbalimbali.
Tazama picha mbalimbali hapa
Rais Mwinyi anasema ni masikitiko yake kwamba hayati Benjamini Mkapa alifariki kabla ya yeye (Mwinyi) kuwa Rais wa amesema anaamini Mkapa angejivunia sana yeye kuwa Rais, kwani matunda ya ulezi wake.
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anasema Hayati Mkapa alikuwa mtu mwenye ‘akili nyingi’, anaeleza kwamba alifanya naye kazi kwa karibu kwenye baraza la Mawaziri chini ya Rais wa wamu ya pili Ali Hassan Mwinyi. Baadae Mkapa akiwa Rais alimteua Kikwete kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hapo ndipo walifanya kazi kwa karibu zaidi.
Kikwete akizungumza katika Kongamano hilo anasema alipogombea Urais mwaka 2005, Mkapa alimuunga mkono na alipokuwa Rais, Mkapa alikuwa kati ya washauri wake wa karibu.
KAMA ULIMISS KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA HAYATI RAIS BENJAMIN MKAPA BASI TAZAMA HAPA MWANZO MWISHO