Top Stories

PICHA 14:Rais Magufuli, Mwinyi, Kikwete na waongoza mazishi ya Hayati Benjamini Mkapa Mtwara

on

NI July 29, 2020 ambapo yamefanyika mazishi ya Rais mstaafu Mheshimiwa, Benjamini William Mkapa nyumbani kwao Lupaso mkoani Mtwara.

Mazishi ya Mhe. Benjamini William Mkapa yamefanyika kwa taratibu za kidini na heshima zote za kijeshi ambapo ibada ya  Mazishi imeongozwa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga ( Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la mazishi la Mbeya) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)  limefanyika gwaride la mazishi likiambatana na kupiga mizinga 21 kwa heshima ya Rais Mstaafu na Amri Jeshi Mkuu wa Awamu ya Tatu.

Viongozi mbalimbali wamehudhuria mazishi hayo wakiwemo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Bombe Magufuli,  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali.

Sasa hapa nimekuwekea picha 14 ujionee mazishi yalivyofanyika ya Hayati Benjamini William Mkapa huko kwao Lupaso mkoani Mtwara.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

MWANZO MWISHO MIZINGA 21 YA KIJESHI IMEPIGWA KWA HESHIMA YA HAYATI BENJAMINI WILLIAM MKAPA ITAZAME HII VIDEO HAPA

SIMANZI:MAMA ANNA MKAPA AWEKA MASHADA KWENYE KABURI LA HAYATI BENJAMINI WILLIAM MKAPA ITAZAME HII VIDEO HAPA

 

Soma na hizi

Tupia Comments