Michezo

PICHA 5: Barcelona wamtambulisha Martin Braithwaite

on

Club ya FC Barcelona ya Hispania leo imemtambulisha Martin Braithwaite kama mchezaji wao mpya ikiwa ni siku moje imepita toka watangaze kukamilisha usajili wake kutokea Leganes kwa mkataba wa miaka minne, Martin Braithwaite amesajiliwa kama mbadala wa Ousmane Dembele ambaye yuko nje ya uwanja kwa miezi sita.

LaLiga waliruhusu Barcelona kufanya usajili huo nje ya dirisha dogo kwa sababu Dembele ni majeruhi na atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitano, sheria ya LaLiga inaruhusu club kusajili nje ya dirisha la usajili iwapo tu mchezaji wake aliyeumia atakuwa majeruhi kwa zaidi ya miezi mitano na anayesajiliwa atatakiwa kuwa huru au mchezaji kutoka ndani ya LaLiga/Hispania.

VIDEO: MECKY AGOMA KUMTUPIA ZIGO LA LAWAMA TINOCO KIPIGO CHA 1-0 CHA SIMBA

Soma na hizi

Tupia Comments