Nyumba 19 zimeteketea kwa moto katika kitongoji cha Shaurimoyo kijiji cha Nyamwage Kata ya Mbwara, Rufiji Mkoani Pwani huku chanzo kikiwa ni Mwananchi mmoja kuwasha moto kwa ajili ya kusafisha eneo lake na kisha moto huo kuzidi na kumshinda kuuzima.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge na Wajumbe wa kamati ya usalama ya Wilaya ya Rufiji wamefika kwenye eneo la tukio ili kuona athari na jitihada ambazo Uongozi wa Wilaya wamezichukua kuhakikisha Wananchi wanakuwa salama ambapo hata hivyo mbali na Wananchi kukosa makazi yao hakuna aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na moto huo.
RC Kunenge ametoa pole kwa Serikali ya Wilaya na Wananchi waliopatwa na moto huo hayo na kuwapongeza Wakazi wa maeneo ya karibu kuweza kuwapatia hifadhi Wananchi wenzao, Kunenge ameuagiza Uongozi wa Wilaya hiyo kufanya haraka kujua tathmini ya athari iliyopatikana ili kuweza kuwasaidia waliopata ajali hiyo.
FAMILIA YA HAMZA YATOA KAULI BAADA YA MAZISHI “MUNGU AMLIPE, KAMA KUNA DENI”