Habari za Mastaa

Picha 7:Nandy akifunguka kuhusu Nandy Festival inayotarajiwa kufanyika DAR

on

Ni Msanii kutokea Bongo Flevani, Nandy ambae leo Agosti 27, 2021 amekutana na waandishi kuelezea maandalizi ya tamasha la Nandy Festival linalotarajiwa kufanyika Dar es Salaam.

Nandy akizungumza na waandishi wa alisema Tamasha hilo litafanyika Mwezi  Septemba 4, 2021 katika viwanja vya Posta.

“Dar ndio kilele kikuu na Dar ndio tunapoishi kwahiyo nikaona sio mbaya mwaka 2019 sikufanya Dar kutokana na bajeti ilikata lakini ninafuraha sana sana mwaka huu naifanya Dar Nandy Festival, hapa nimezungukwa na wadhamini na walikuwa wakitamani iende nje ya Tanzania lakini tunawapa heshima wakazi wa DAR”- Nandy

.

“Kuna watu wameshafanya Tamasha karibia miaka 20 sasa lakini mimi ndio kwanza mwaka wa pili sijui vingi na kila mtu katika tamasha lake ana silaha zake ili kufanikisha tamasha lake nikiwa kama mwanamke, msanii mdogo ambae ninae pambana kwa ajili ya kwangu, timu yangu na Mashabiki wangu na watu wanaopata ajira kupitia Nandy Festival kiukweli tunapitia mazito sana”- Nandy

.

“Kuna Suprise ya wasanii kutoka nje ya nchini zikiwemo Nairobi, US na Nigeria muda sahihi utakapofika tutawataja majina yao, ikumbukwe kwamba 2019 sikuwa nawadhamini hata mmoja nilifanya Nandy Festival kwa nia njema kwamba najua mwaka utakaofuata wadhamini wataona,  nilichokifanya na nyie waandishi mmeshuhudia mwaka huu tulivyopata wadhamini na wamefanya tamasha hili kwa upande mwingine lile rahisi”- Nandy

.

.

.

.

NANDY AMEFUNGUKA SABABU YA KUFANYA MAANDAMANO ATANGAZA KUBWA HILI

 

 

 

 

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments