Leo Ayo TV na Millardayo.com inakusogezea picha mbalimbali zilizopigwa katika baadhi ya barabara za jijini Dar es Salaam juu ya usalama wa watumiaji wa usafiri wa Pikipiki maarufu kama ‘Bodaboda’.
Picha hizi zimepigwa kuanzia majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana katika maeneo ya Mlimani City, Mbezi Africana na Mikocheni.
Hata hivyo katika picha hizi zilizopigwa na Mpiga Picha wetu &zuch zimeonyesha abiria mmoja kati ya 13 ndiye aliyevaa kofia ngumu ‘Helment’.
Licha ya jeshi la Polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kuendelea kutoa elimu kwa madereva bodaboda na abiria juu ya umuhimu wa kuvaa kofia ngumu (helmets) wakati wa safari, bado somo hilo limeonekana kutokuzaa matunda kwa madereva na abiria wanaotumia usafiri wa bodaboda.
Kupitia picha hizi kundi la abiria wanawake limeonekana kuongoza kwa kutokuvaa kofia ngumu (helmets) ukilinganisha na abiria Wanaume.
Ayo TV na Millardayo.com inapenda kuwakumbusha abiria wote na maderera wanaotumia usafiri wa bodaboda kujilinda kwa kuvaa kofia ngumu pindi wanapotumia usafiri huo ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea wakati wa ajali.