Balozi wa china nchini Tanzania Chen Mingjian amesema mahusiano yalioachwa na waasisi wa mataifa hayo mawili Mwl. Julius Nyerere na mao Tse Tung ndio msingi wa ushirikiano katika maendeleo ya nchi hususani katika ujenzi wa miundombinu ya kimkakati inayofanyika nchini Tanzania.
Balozi Chen Mingjian ameyabainsha hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Daraja la JPM kati ya Kigongo na Busisi, mradi unaojengwa na Kampuni ya CCECC ya nchini China kwa gharama ya zaidi ya Tsh. Bilioni 716.
Mara baada ya kukagua ujenzi Daraja la JPM, Balozi Mingjian pia ametembelea na kujionea ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha tano kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga, ambapo pia mradi huo unajengwa na kampuni ya CCECC ya nchini China.
Geofrey Mwambe Mbunge wa Masasi Mjini ni miongoni mwa Wabunge marafiki wa Bunge la China ameeleza wao wanaamini kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na China unaleta tija katika maendeleo ya Taifa kwa ujumla.