Jumla ya Shilingi bilioni 120 zimetumika kuboresha sekta ya afya, miundombinu na michezo Jiji la Dar es salaam kupitia mradi wa uendeshaji wa jiji la Dar es salaam (DMDP)
mradi huo unaotekelezwa na DMDP chini ya usimamizi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) umewezesha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami , masoko, magari taka, visima vya maji, vyoo vya umma, stand ya mabasi na madaraja
“Ilala tulipokea Sh. bilioni 120 kati ya bilioni 600 zilizotolewa kama mradi kwenye Jiji lote la DSM, kupitia kiasi hicho cha pesa tumetengeneza barabara kilomita 41, masoko 3, magari matano ya taka, visima vya maji 10, vyoo vya umma vitatu na madaraja, eneo la mapumziko, stand ya kisasa “ Selestina Lyugasila mratibu msaidizi DMDP Ilala