Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini Mheshimiwa Abdul Aziz Abood amegawa viakisi Mwanga 1500
Kwa madereva pikipiki mjini Morogoro vyenye ujumbe wa kutangaza Filamu ya The Royal Tour.
Mheshimiwa Abood amesema kua lengo la kugawa viakisi mwanga hivyo vyenye ujumbe huo ni jitihada za kuunga mkono serikalini kukuza sekta ya utalii.
Amesema Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan ameonesha Mwanga kuhamasisha utalii hivyo ni lazima wasaidizi wake kuunga mkono juhudi hizo
Abooda anasema madereva Bodaboda ni kundi kubwa hivyo kupitia kundi hilo ujumbe utafika sehemu kubwa kwani wao wanakutana na watu wa aina mbalimbali ikiwemo raia kigeni.
Aidha Mhe. Abood amewataka Bodaboda hao kuunda vikundi ili kupata mkopo wa asilimia 4 wa vijana unaotolewa na halmashauri ili wajipatie kipato kitakacho waiunua kiuchumi.
Kwa upande wake mmoja wanufaika Ally Yusuph amemshukuru Mbunge Abood Kwa jitihada zake za kuwajali kundi hilo.
Anasema madereva wengi wamefariki Kwa kugongwa na magari kutokana na kukosa viakisi Mwanga hivyo upatikaji wake utasaidia kupunguza ajali huku wakiahidi kutangaza utalii