Chuo cha Mafunzo ya Ukarabati na matengenezo ya Barabara cha Chuo cha mafunzo ya Teknolojia Ujenzi stahiki ya nguvukazi ICOT cha mkoani Mbeya kimesaidia Serikali kuokoa zaidi ya shilingi milioni 45 kwa kutengeneza Barabara kwa kutumia wahitimu wa Kozi ya teknolojia Ujenzi stahiki ya nguvukazi kwa Wanawake, vijana na wazee kwenye Barabara ya changarawe ya urefu wa mita 980.
Hayo yamesemwa na Meneja TARURA Mkoa wa Mbeya Eng. Wilson Mwita alipokuwa akikagua ilikufungua Barabara ya Ilamba – Itekele kijiji cha Kikota Kata ya Kiwila Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya iliyojengwa teknolojia stahiki ya nguvukazi kwa Wahitimu wa Kozi ya vikundi maalumu vya Wanawake, vijana na wazee ya mwezi mmoja na kozi ya wiki 10.
Eng. Mwita amesema ubora wa Barabara hiyo Chuo hicho pia kimesaidia toa mafunzo ya kutengeneza Barabara za vijijini kwa makundi hayo ya Wanawake, vijana na wazee kimesaidia kumaliza tatizo la ukosefu wa Barabara kwa wakazi wa Ilamba – Itekele.
Amesema Barabara hiyo kwa jinsi anavyoiona itahitaji matengezo baada ya miaka mitano hadi sita ijayo.
Mkuu wa Chuo cha mafunzo ya teknolojia Ujenzi stahiki ya nguvukazi cha ICOT Mbeya Eng. Mahmoud Chamle akielezea Barabara hiyo amesema Chuo hicho kimejikita sana na Ujenzi wa Barabara kwa Teknolojia ya Ujenzi stahiki ya nguvukazi kwa makundi mbalimbali ya Wanawake, Vijana na wazee ili waweze kusaidia taifa kuongeza mtangao wa Barabara zenye ubora hadi vijijini.
Amesema Barabara hiyo ilivyojengwa amesema malighafi zilizotumika kutengeneza Barabara hiyo zote ni rasilimali kutoka ndani ya maeneo ya Ilamba – Itekele.
Naye Msimamizi wa Kozi hiyo Donata Kamwela amesema katika Mahafari hayo kulikuwa na Wahitimu wa Kozi ya vikundi maalumu ya mwezi mmoja ambayo ilikuwa na Wahitimu 24 na kozi ya wiki 10 ambayo ilikuwa na Wahitimu saba.
Hatahivyo Mshiriki wa Mafunzo hayo Frola Makhota amemuomba TARURA nchini kutoa kazi kubwa za ujenzi wa Barabara kwa kundi hilo lililopata Mafunzo hayo bila kuwabagua na kuendelea Wakandarasi wakubwa wenye mitambo kwa Barabara za kutengenezwa kwa changarawe na udongo.