Ni Mei 28, 2022 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ameungana na wenyeviti wa kata na watendaji katika zoezi la kusafisha mitaro mbalimbali.
Aidha DC Jokate ameagiza TARURA kuendelea kuhakikisha miundombinu ya wilayani humo inakuwa katika hali ya usafi na salama kuepuka magonjwa mbalimbali ya milipuko.
‘Kwanza nashukuru wenyeviti na madiwani kwa kujumuika siku ya leo hii iwe muendelezo isiishie tu leo lengo kuifanya Temeke inakuwa katika hali ya Usafi na maeneo mengine kupendeza’- DC Jokate
‘Kwa mfano ukipita pale nje ya Uwanja wetu wa Benjamin Mkapa hali ya zamani na sasa ni tofauti zimefungwa taa 32 nzuri pamependeza kwahiyo natoa rai maeneo mengine tushirikiana na TARURA ili Temeke iwe namba moja kwa usafi’- DC Jokate