Kamati ya bajeti ya bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wake Daniel Baran Sillo yaridhishwa na Ujenzi wa Shule shikizi (Kaza Roho) uliogharimu Milioni 120 Babati Mkoani Manyara.
Kamati hiyo ya Bajeti imeambatana na wajumbe mbalimbali wakiwemo Halima Mdee,Ester Matiko na Tarimba Abas,shule hiyo ilianzishwa mwaka 2018 ambapo kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19 yamejengwa Madarasa 6.
Shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nyumba za waalimu,huduma ya Maji pamoja na upungufu wa waalimu ambapo Kamati imeahidi kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.