Top Stories

Picha 11 kubwa za dunia kwa mwaka 2019.. Afrika Mashariki ipo moja

on

Picha hizi 11 ni sehemu ya orodha ya picha zilizotajwa na Television ya ABC Marekani kwamba ni moja ya picha kubwa za dunia kwa mwaka 2019 zikiwa zimepigwa kwenye mataifa mbalimbali.

Wanafamilia wa Kipalestina wakipata mlo wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani pembeni ya jengo lililoharibiwa wakati wa mashambulizi kati ya Hamas na Israel May 18 2019. (credits: Mahmud Hams/AFP/Getty Images)

Miili ya Mhamiaji kutoka Salvador Oscar Alberto Martinez Ramirez na Mtoto wake wa kike aliekua na zaidi ya mwaka mmoja, ikiwa pembeni ya Mto Brownsville Texas Marekani ambako walikua wanajaribu kuvuka kuingia Marekani kutafuta maisha bora, Mke wake alisema alishuhudia Mume wawili hao wakisombwa na maji yenye nguvu. (credits: Julia Le Duc/AP)

Aliana Alexis akiwa amesimama sehemu ilipokuwepo nyumba yake ya kuishi, yanayoonekana ni mabaki baada ya kimbunga Dorian kutokea Great Abaco Island, Bahamas Sept. 5. kusababisha vifo vya Watu 50 pamoja na uharibifu. (credits: Al Diaz/Miami Herald/Tribune News Service via Getty Images)

Polisi akimtisha Muandamanaji Hong Kong Aug. 25, 2019 ambapo pamoja na kunyooshewa Bastola, Muandamanaji huyo hakuondoka bali alitanua mikono yake miwili na kuonyesha utayari kwa lolote. (credits:Lam Yik Fei/The New York Times via Redux Pictures)

ZAMBIA: Watu wakikimbia baada ya kupokea msaada wa chakula kutoka kwenye Helikopta ya Jeshi la South Africa ambayo ilikua ikikagawa msaada kwenye eneo hilo lililokua na mapigano. (credits: Siphiwe Sibeko/Reuters)

Mtoto wa kike wa Syria akisubiri kuokolewa baada ya kupona kwenye shambulio la anga huko Khan Sheikhun Syria, hapo alipo yupo karibu kabisa na mwili wa Dada yake ambae alifariki kutokana na shambulio hilo. (credits: Anas Al-Dyab/AFP/Getty Images)

Mwanamke Mhamiaji kutoka Guatemala Ledy Perez akiwa na Mtoto wake akilia na kuomba mbele ya Mwanajeshi ili aachiwe kupita kuingia Marekani kwenye mpaka huo na Mexico July 22 2019. Wawili hao walikua wamesafiri umbali wa mile 1500 mpaka kufikia hapo na walikua wamebakiza hatua chache tu kuingia Marekani ambako wanaamini maisha yao yatapata unafuu. (credits:Jose Luis Gonzalez/Reuters)

October 29 2019 Marekani, Maboss wa kampuni ya kutengeneza Ndege ya Boeing wakiwa wamegeuka kuwatazama baadhi ya Watu waliokua wamebeba picha za Ndugu zao ambao walipoteza maisha baada ya ajali mbili za Ndege za Boeing aina ya 737 max zilizoua Watu 346. (credits: Sarah Silbiger/Reuters)

Baadhi ya Watu wakiwa nyuma ya Askari wa Kenya baada ya milio ya risasi kusikika kwenye Hoteli moja ya kifahari Nairobi Kenya, shambulio hilo lilifanywa na Al-Shabaab na lilisababisha vifo vya Watu 21 lakini Wanajeshi wa Kenya walisifika kwa kuwahi eneo la tukio na kuepusha maafa zaidi. (credits:Baz Ratner/Reuters)

Mtengeneza Mask wa China akiwa na mask aliyoitengeneza yenye sura ya Rais Donald Trump wa Marekani. (credits: Wang He/Getty Images)

Mwalimu Jiang Tongying (56) akicheza na Watoto anaowafundisha kwenye Shule ya Msingi huko China ambapo amekua Mwalimu kwenye Shule hiyo toka mwaka 1982. Baadhi ya Walimu wapya ambao wamekua wakipangiwa kufundisha kwenye Shule hiyo huondoka baada ya muda mfupi kutokana na mazingira magumu ya kazi na maisha kwenye eneo hilo. “Napenda Watoto, nataka kuwa Mwalimu wa hii shule milele” (credits:Yang Wenbin/Xinhua via Newscom

MUME KAENDA KAZINI, WIFE KALETA MCHEPUKO NYUMBANI

FULL INTERVIEW: MTOTO GUMZO ANTHONY KAZUNGUMZA TUSIYOYAJUA

Soma na hizi

Tupia Comments