Zimebaki saa chache kwa CHADEMA kufanya mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho ambao Wajumbe wa mkutano huo leo Januari 21, 2025 wanatarajia kuchagua mwenyekiti wa chama na makamu wenyeviti wa Bara na Zanzibar, ambapo ushindani mkali upo kati ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Makamu wake, Tundu Lissu wanaogombea uenyekiti.