Michezo

PICHA: Kwenye Ndondo Cup leo June 10 2019 uwanja wa Kinesi

on

Michuano ya Ndondo Cup 2019 inaendelea katika viwanja vya Bandari na Kinesi wilaya ya Ubungo, ambapo uwanja wa Kinesi leo mambo yalikuwa magumu kwa timu zote mbili sio Ilala United wala Uruguay waliofanikiwa kuondoka na point tatu.

Mchezo huo ulikuwa mgumu na ushindani mkubwa na kila timu ilionekana kuwa makini zaidi na kutotaka kuruhusu goli hususani dakika za awali, hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilimalizana kwa kutoka sare tasa (0-0) na kugawama point moja moja.

Kwa upande wa uwanja wa Bandari ambapo ilipigwa game mmoja pia kati ya Millenium na Makuburi, game hiyo ilimalizika kwa Millenium kupata point tatu kwa ushindi wa goli 1-0, June 11 2019 zitachezwa game mbili tena katika uwanja wa Bandari ni Gobaham dhidi ya Uv Temeke na uwanja wa Kinesi ni Mpakani Kombaini dhidi ya Ukwamani.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments