Kampuni ya mabingwa wa vifaa vya kielektroniki Haier wamefanya mkutano wa uzinduzi wa bidhaa za viyoyozi (AC) katika ukumbi wa Hyatt regency, the kilimanjaro hotel, jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 19.04.2024.
Mkutano huo ulihudhuriwa na, wadau na watumiaji wa bidhaa za kielekroniki wakiwemo wataalam mbalimbali wa ujenzi, wasanifu majengo, wafanyabiashara wa vifaa vya kilektroniki, taasisi mbalimbali za kiserikali na wafanyakazi wa makampuni ya GSM GROUP pamoja na Haier.
Kampuni ya Haier iliingia rasmi ubia na kampuni ya GSM GROUP mnamo mwanzoni mwa mwaka 2023. Kwa kipindi hiki chote, kampuni ya Haier ikishirikiana na GSM GROUP imekuwa ikihakikisha inaleta bidhaa ambazo zina tija sokoni.
‘Tangu uanzishwaji wa kampuni ya Haier, Tanzania, tumekuwa tukijitahidi kuangalia matakwa ya soko na kuhakikisha tunaboresha huduma na ufanisi wa bidhaa zetu kwa watumiaji’ Alisema haya meneja biashara, Bw. Ibrahim Kiongozi.
Sambamba na uzinduzi huo wageni waalikwa walipata nafasi ya kujionea bidhaa hizo mpya na kupata mafunzo mafupi kwa ajili ya matumizi ya vifaa hivyo.
‘Sifa kubwa za bidhaa hizi za AC ni mfumo wake imara na wa kisasa unaosababisha matumizi kidogo ya umeme pamoja na uwezo mkubwa wa utendaji kazi katika kutoa hali ya ubaridi kwa haraka.’
Aliongezea Meneja mkuu kutoka Haier, Bw. Leon Liuchi. Ushirikiano wa makampuni ya GSM Group na Haier unaleta tija katika ukuaji wa uchumi wa nchi kutokana na mapato na ajira mbali mbali zinazotolewa.
‘Katika kuhakikisha kwamba GSM GROUP ikishirikiana na Haier inaungana na juhudi za kukuza uchumi wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan, tunajitahidi kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii zikiwemo udhamini wetu katika michezo kupitia timu mbali mbali za mpira wa miguu kama Young Africans Sports Club (Yanga), Coastal Union, Singida Fountain Gate na Ihefu’ Alisisitiza, Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya GSM Group, Mr. Benson Mahenya.
Vile vile katika mkutano huo, wageni waalikwa walipata fursa ya kujishindia bidhaa za jokofu (fridge) pamoja na kiyoyozi (AC).
Uongozi wa makampuni ya GSM GROUP na Haier ulitoa shukrani kwa wadau mbali mbali walioshiriki pamoja na kuahidi kuendeleza ubunifu kwa matoleo ya mbeleni ya bidhaa za kielektroniki Tanzania. Vilevile Haier imethibitisha kuongeza mpango kazi katika kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa hizo mikoa yote ya Tanzania.