Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango leo Machi 16, 2022 amezindua daraja lenye urefu mita 84 lililopo katika kata ya Magara Wilaya ya Babati Mkoani wa Manyara.
Daraja hilo mpaka kukamilika kwake limegarimu shilingi Bilioni 12 ambapo litahudumia wakazi wanaoelekea barabara kuu ya Dodoma, Mbulu na Karatu.
Daraja hili ni kiungo muhimu kwa wakazi wa Mkoa wa Manyara na maeneo ya jirani ambapo awali Wananchi walikuwa wakishindwa kuvuka na kupelekea baadhi ya wananchi kupoteza Maisha.