Michezo

PICHA: Man City walivyosherehekea Ubingwa wao wa EPL

on

Man City wamefanikiwa Kutwaa Ubingwa wa EPL baada ya ushindi mnono, Man City anatwaa Ubingwa huo kwa point 93 dhidi ya Liverpool wenye point 92 ambazo wamezipata baada ya ushindi wa leo wa 3-1 dhidi ya Wolves.

Hadi dakika 70 Man Ciyu walikuwa nyuma kiasi cha wengi kuamini kuwa Man City anachia Ubingwa huo, wakati ambao Aston Villa walikuwa mbele kwa magoli Cash dakika ya 37’ na Coutinho dakika ya 69.

Ziliwachukua dakika 7 tu Man City kupindua meza kwani dakika ya 76 Gundogan akapachika goli la kwanza na Rodri kufunga la pili dakika ya 78 kabla ya Gundogan kurudi tena dakika ya 81 kuhitimisha shughuli yao ya Ubingwa na kuufanya mchezo kumalizika kwa ushindi wa 3-2.

Msimamo wa EPL msimu wa 2021/2022 ndio umemalizika hivi.

Matokeo ya mechi za mwisho wa msimu EPL

Soma na hizi

Tupia Comments