Timu ya Taifa ya Argentina leo alfajiri kwa saa za Argentina wamewasili Buenos Aires wakiwa na Kombe la Dunia.
Pamoja na kuwa wamewasili alfajiri lakini maelfu ya mashabiki wa Argentina wamekesha wakiisubiria kuwasili kwa timu hiyo ambayo imetwaa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.
Hata hivyo pamoja na leo Jumanne kuwa siku ya kazi serikali ya Argentina ili kutoa fursa ya kusherehekea, leo imetangazwa kuwa siku ya mapumziko.