Michezo

PICHA: Mapokezi ya Timu ya Taifa ya Guinea ikitokea CHAN Cameroon

on

Timu ya Taifa ya Guinea imerejea nchini Guinea katika mji wa Conakry na kupata Mapokezi Makubwa kutoka kwa mashabiki wa soka nchini humo licha ya kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya CHAN 2020 iliyomalizika nchini Cameroona kwa Morocco kuwa Bingwa.

Guinea walimaliza nafasi ya Mshindi wa tatu kwa kumfunga mwenyeji Cameroon kwa magoli 2-0, hata hivyo Guinea walikuwa na hamasa kubwa toka mwanzo wa mashindano kwani Rais wa Chama cha soka nchini Guinea na mmiliki wa Klabu ya AC Horoya Antonio Souare alileta mashabiki 190 kutoka Guinea kuisapoti timu yao nchini Cameroon.

Guinea kama utakumbuka walikuwa Kundi D na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars pamoja na Namibia na Zambia, hata hivyo katika mchezo wao dhidi ya Taifa Stars ulimalizika kwa sare ya 2-2 baada ya Guinea kusawazisha wakitokea nyuma na kuifanya Tanzania iage mashindano hayo.

Soma na hizi

Tupia Comments