Meya wa Jiji la Mwanza Sima Constantine amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kumchukulia hatua kali za kisheria Mhandisi wa Jiji alitoa vibali kinyume na taratibu za Mipango Miji kwa Wamiliki waliojenga vibanda holela na kupelekea kuziba vichochoro kati kati ya Jiji la Mwanza.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Meya aliyoifanya maeneo mbalimbali Jiji, ikiwemo mtaa wa Deluxe na kukuta ujenzi holela ukiendelea bila kufata taratibu za Mipango Miji.
Sima anaeleza kuna baadhi ya Wahandisi wa Jiji wamekuwa wakiendelea kuwa kwamisha kwa kutoa vibali kwa Wamiliki na kuruhusu Ujenzi uanze bila kufuata mpangilio wa Jiji unavyoelekeza kwa Wamiliki kufanya ujenzi rasmi.
Ameongeza kwa kusema Wamiliki wote waliojenga kiholela wapewe Note’s na uvunjwaji wa majengo yao ufanyike mara moja huku akisisitiza kuanza kwa operasheni maalumu ya kuondoa vibanda vilivyoziba Barabara kati kati ya Jiji.