Ni Machi 26, 2023 ambapo Millardayo.com & Ayo TV inakukunisha na stori ya Mfugaji Mariam Mwipasya ambae ni Mkazi wa Isanu Wilaya ya Busokelo Mkoani Mbeya.
Ambae amefunguka yale tusiyoyajua kuhusu Ufugaji wake mpaka namna alivyopata faida alipoanza kufanya kazi na Kampuni ya Asas.
“Nimefuga Ngombe kwa muda mrefu na Mwanzo tulikuwa tunashida ya Maziwa tulikuwa tunashindwa sehemu yakuyauza maziwa tulikuwa tunayapeleka Ipinda na kuyamwaga maziwa yalikuwa hayafanyi vizuri”- Mariam Mwipasya
‘Kindoo tulikuwa tunauza Elfu 5 ama Elfu mbili lakini kwasasa tulivyoanza kufanya kazi na Asas tunapata faida kubwa na tunafuga Ng’ombe kwa faida tunajua kila tarehe 15 tuna hela kwani kwa Mwezi tunapata mara mbili sasa tunamshukuru sana Ahmed kwa kutupatia mitaji ya kufanya kazi vizuri na kufunga kwa tija”- Mariam Mwipasya
“Kila tarehe 15 sipungukiwi kupata laki tatu na tarehe 30 hivyo hivyo kwa mwezi napata laki saba mpaka laki nane, Namshukuru sana Asas nashukuru sana Ahmed kwa kutukumbuka sisi wafugaji na kupitia Kampuni yake imefanikisha na mimi kujenga Nyumba ambayo kwa hapa ilipofika ni hatua kubwa sana”- Mariam Mwipasya
“Ufugaji unafaida kubwa sana pamoja na kusaidia familia yangu hususani watoto wanaenda Shule ni jambo la heri la kutuinua sisi kiukweli asante sana Asas kwa kutukomboa sisi wafugaji maisha yanaendelea”- Mariam Mwipasya