Kamati ya Utekelezaji ikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida imetembelea Maskani ya CCM ya Dkt Mohammed Ali Sheni Iilyopo Wadi ya Jojo Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo imechangia Tsh. Laki tano kwa ajili ya kuunganisha umeme katika Jengo hilo.
Komredi Kawaida amewapongeza Wananchi wa JOJO kwa kujitokeza kwa wingi na kusisitiza uwepo wao ni ishara ya kuwa Uhai wa Chama katika Wilaya ya Wete upo imara.
Aidha Komredi Kawaida amewashukuru sana kwa kuwasihi Wananchi kuendelea kuwaunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi kwa kazi kubwa wanazozifanya za kuwaletea Maendeleo.
Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha Uhai wa Chama cha Mapinduzi na Jumuiya ya Umoja wa Vijana, Kusikiliza hoja na Changamoto za Wananchi na kuzitatua, pamoja na kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya CCM Mikoa ya Pemba ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020 – 2025 pamoja na miradi ya Chama na Jumuiya zake.