Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limezundua mashindano ya Polisi Jamii Cup yenye lengo la kuishirikisha jamii hususani vijana katika kupambana na uhalifu katika mkoa wa Manyara kupitia michezo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Acp George Katabazi amesema wakati wa mashindano elimu itatolewa kwa Jamii kupambana na uhalifu ikiwemo kukata dawa za kulevya,uvunjaji, unyamg’anyi wa kutumia Silaa pamoja na kujichukulia sheria mkononi, ambapo amesema mashindano hayo yanafanyika katika wilaya zote mkoa wa Manyara ikiwa ni agizo la Mkuu wa jeshi la Polisi nchini.
Akizindua mashindano hayo Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Manyara amesema Lengo la mashindano hayo ni kuisogelea jamii kwaajili ya kupambana na uhalifu lakini pia michezo ni afya pamoja na ajira.