Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo hii ameingia siku ya pili ya ziara yake nchini Zambia kwa kutembelea eneo la mashujaa lililopo barabara ya Uhuru Lusaka.
Eneo hilo lilijengwa mnamo mwaka 1974 ikiwa ni miaka 10 tangu nchi hio kupata uhuru.
Aidha katika hatua nyengine mara baada ya kufanya Sala katika kumbukumbu hizo za mashujaa pamoja na kuweka mashada ya maua Rais Dkt Samia Suluhu Hasaan akazuru Kaburi la Rais wa kwanza wa Taifa hilo Kenneth Kaunda.