Michezo

PICHA: Wachezaji wa Azam FC walivyofika kumpa pole Agrey kwa kufiwa na mkewe

on

Wachezaji na viongozi wa Azam FC leo ikiwa ni siku moja imepita toka watolewe katika michuano ya Mapinduzi Cup 2020 na SImba SC kwa mikwaju ya penati 3-2, leo wamerejea jijini Dar es Salaam na moja kwa moja wakaenda kumfariji nahodha wao Agrey Moris.

Viongozi na wachezaji wa Azam FC leo walifika kumfariji mchezaji mwenzao Agrey Moris ambaye amefiwa na mke wake jioni ya Januari 10 akiwa kwenye harakati za kujifungua, mazishi ya marehemu mke wa Moris yatafanyika Jumatatu ya January 13 2020 Kitunda Mwanagati.

VIDEO: TATHMINI YA ALLY MAYAY KUHUSU FAINALI MAPINDUZI CUP, KAULI YA NUGAZ ILIYOMFANYA AOMBE RADHI JE?

Soma na hizi

Tupia Comments