Jaji Mfawidhi mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro , Paul Ngwembe amewataka waandishi wa Habari kuandika habari Kwa Kuzingatia sheria na taratibu za mahakama ili kutoingilia uhuru wa mahakama au utendaji kazi wake
Jaji Mfawidhi Ngwembe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya waandishi wa habari,wahariri pamoja na maafisa habari wa mahakama juu ya kuandika habari za kimahakama ambapo wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii juu ya taarifa zinazohusu mahakama.
Amesema kua waandishi ndio chombo ambacho kinaweza kufikisha elimu Kwa Jamii kwa haraka kuhusu utendaji kazi wa mahakama hivyo wanawajibu katika kutoa elimu juu ya sekta hiyo .
Anasema Jamii bado inahitaji elimu kuhusu masuala ya utambuzi wa sheria Hivyo uandaaji wa habari za kimahakama umekua changamoto Kwani zimekua zikileta taharuki Kwa wananchi.
Mafunzo hayo ya siku nne yameratibiwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yalifunguliwa jana na Jaji Mfawidhi Mhakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro ambapo amesema waameamua kutoa mafunzo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuripoti habari za kimahakama kwenye jamii zinazowazunguka.
Aidha Jaji Mfawidhi Ngwembe ametoa wito Kwa wadau wa mahakama ikiwemo ofisi ya mwanasheria kutumia mfumo tehama ili kuharakisha utolewaje maamuzi ya mashauri Kwa haraka.
Kwa upande wa wakazi wa Morogoro wamepongeza jitihada za mahakama namna ya kutoa Elimu ambapo kupitia vipindi mbalimbali vinavyofanywa kupitia vyombo vya habari wamekua wakielimika na kutambua haki za wananchi.