Top Stories

Picha: Waziri Makame afanya ziara katika mradi wa Mabasi yaendayo haraka DSM

on

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Makame Mbarawa amefanya ziara katika Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Jijini Dar es salaam.

Ziara hiyo ilianza barabara ya Kilwa hadi Mbagala na kupitia katika Barabara ya Juu sehemu ya Uhasibu ambapo alieleza kwamba ameridhika na maendeleo ya mradi na kuahidi wananchi wanayotumia njia hii mpaka ukifika Mei 30, 2022 upande moja wa Barabara ya Juu utakua imekamilika na itafunguliwa ili ianze kupitisha magari.

.

Waziri Mbarawa alifafanua kwa kusema Barabara itakapo funguliwa itatumika kwa ratiba maalum nayo ni asubuhi wakazi wa Mbagala watumia barabara ya Juu kuwawezesha kuenda mjini kufanya shughuli za kiuchumi na jioni Daraja la juu litatumika na wananchi kutoka mjini kuelekea Mbagala.

.

Waziri amesema Anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha fedha zote za Mradi kulipwa kwa Wakati na yeye Kama Waziri anayohusika na maswala ya miundombinu atahakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi. Alimalizia kwa kuahidi kwamba tarehe 30 Mei mradi wa Wami pia utaanza kupitisha magari.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

,

.

Tupia Comments