Siku mbili baada ya kukutana na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mratibu wa Kimataifa wa Mpangobwa Dharura wa Rais wa Marekani katika mwitikio wa kupambana na UKIMWI (PEPFAR) Dkt. John Nkengasong, ametembelea Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU Tanzania (NACOPHA)na kuongea na makundi mbalimbali ya Vijana, ikiwa ni pamoja na majukwaa ya Vijana kutoka Vyuo vikuu, Shule za Sekondari, Mitandao ya vijana wanaoishi na VVU, na makundi tofauti ya Watu wanaoishi na wanaoishi na VVU (WAVIU).
Dkt. Nkengasong ameongea na Vijana wanaoishi na VVU na kuelewa changamoto zao, pamoja na kutambua maeneo ya kuboresha ili kuimarisha huduma za VVU huku akipongeza mikakati ya Vijana na kuahidi kusaidia kuunda Bodu ya Ushauri ya Vijana ili kuwahusisha katika uundaji wa sera na mipango mikakati ili kufikia malengo yaliyowekwa ili kuweza kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030.
Dkt. Nkengasong amesema kuna umuhimu wa kuwajumuisha Vijana kwenye mipango mbalimbali “Hakuna kitu kwa Vijana bila Vijana wenyewe (Nothing for the youth withouth the youth) “
Vijana pia walipata nafasi ya kuelezea haja ya mapitio ya sera ili kuunda mazingira rafiki kwa utoaji na upatikanaji wa huduma za VVU, huku wakisgukuru kwa ugeni huo na pia msaada waliopokea kutoka serikali ya Marekani kupitia PEPFAR, pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.