Habari za Mastaa

Baada ya stori za Dudubaya kumkata sikio, Mama mwenyewe amejitokeza kuthibitisha

on

Screen Shot 2014-04-11 at 5.28.49 PMSiku mbili zilizopita stori mbalimbali kwenye mitandao zilihusu msanii wa longtime kwenye bongofleva aitwae Dudubaya kudaiwa kumkata sikia Mama yake mkubwa kwa kinachosemekana kuwa tuhuma za kichawi lakini siku moja baadae Dudubaya alikanusha kupitia U Heard ya XXL Clouds FM kwamba hajamkata bibi yake sikio, yeye sio mtu wa kufanya hicho kitendo.

Sasa leo Mama mkubwa huyu wa Dudubaya amezungumza na Waandishi wa habari na kuthibitisha kweli kukatwa sikio na Dudubaya ambapo shahidi mwingine aliezungumza ni mjukuu wake.

Maelezo waliyoyatoa ambayo ndio yamenifikia sasa hivi yatawekwa hapa on millardayo.com baadae lakini pia yatasikika kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kuanzia saa moja leo usiku.

Ili kupata kila kitakachotokea, kaa karibu na mimi kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo ili nikutumie taarifa baadae.

Screen Shot 2014-04-11 at 5.03.37 PMSehemu aliyokatwa imezibwa kwa makusudi.

Screen Shot 2014-04-11 at 5.04.02 PM

Screen Shot 2014-04-11 at 5.03.20 PM

Screen Shot 2014-04-11 at 5.03.14 PM

Tupia Comments