Leo, Januari 27, 2025, mkutano muhimu wa nishati unaowakutanisha Mawaziri wa Nishati, Mawaziri wa Fedha, na wadau wa maendeleo unafanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mkutano huu, unaojulikana kama “Mission 300”, unalenga kujadili mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati kwa watu milioni 300 barani Afrika.
Viongozi mbalimbali, wakiwemo Wakuu wa Nchi za Afrika, wanahudhuria mkutano huu.
Mawaziri wa Nishati 60 wanashiriki katika mkutano huo ambao umefunguliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.