Top Stories

Picha:Rais Mwinyi awaapisha Makatibu Ikulu Zanzibar

on

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ally Mwinyi  Agosti, 2, 2021 amewaapisha Makatibu Wakuu mbali mbali aliowateua Julai 30 Mwaka huu kushika nyadhifa hizo.

Katika hafla ya uapisho uliofanyika Ikulu visiwani Zanzibar Dk.Mwinyi amemuapisha Dr.Omar Dadi Shaak kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar pamoja na Bi. Khadija Khamis Rajab kuwa Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Kazi na uwezeshaji katika Wizara ya Nchi (OR) katika, Uchumi na Uwekezaji.

Aidha, amemuapisha Dk.Habiba Hassan Omar kuwa Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Uchumi na Uwekezaji katika Wizara ya Nchi (OR) Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Mwingine alieapishwa ni Dk,Fatma Mrisho kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Katika hatua nyingine, Mh Rais Dk. Hussein Mwinyi amemuapisha Ndugu Khamis Kona Khamis kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar, kufuatia uteuzi wake wa tarehe 16 Julai 2021.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

MBUNGE WA CCM AJIUZULU, CHAMA CHATOA MSIMAMO “SUALA LA KIFAMILIA”

AMBULANCE MBILI ZA BOTI, ZITATOA HUDUMA NDANI ZA ZIWA VICTORIA

 

Soma na hizi

Tupia Comments