Leo March 11 2017 nchini Tanzania imewasili Treni ya Kifahari ya Kitalii ya Rovos Rail Treni ikiwa na jumla ya watalii 71 ambao waliiambia Ayo TV na millardayo.com kuwa walianza safari yao kutoka South Africa March 1 2017.
Kwa mujibu wa msemaji wa Treni hiyo akizungumza na Ayo TV, amesema katika safari yao wamepita nchi za Botswana, Zimbabwe, Zambia na leo March 11 2017 ndio wameingia rasmi Tanzania.
‘Ni safari ambayo tumeianza March 1 2017 na leo March 11 2017 tumeingia Tanzania. Tunatarajia kuzifanya safari hizi mara tano kwa mwaka na hii ya leo ndio safari yetu ya kwanza‘ – Querida Vented.
Ulimiss OnAIR ya Irene Uwoya: Ataemchukulia Uwoya Mwanaume, Wanaume wanaokwenda Saluni je? itazame hii video hapa chini…