Mix

Saa 48 alizozitoa Waziri wa Magufuli kwa Wauza ‘Unga’…(+Pichaz)

on

Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga amefanya ziara ya ghafla leo Dec 16 2015 katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Polisi Dar es salaam na kutoa amri kwa viongozi wa jeshi hilo siku mbili za kuhakikisha amepata taarifa kuhusu  udhibiti wa dawa za kulevya.

Wapo wajanja wana mbinu nyingi, lakini hawawezi kutuua. Na mimi hili ni jambo nitalivalia njuga, lakini kwanini katika ukamataji wa dawa za kulevya sisi tulioko kwenye operesheni tunakaa pembeni? Nataka jibu siku ya Ijumaa

Kuhusu watu kubambikiziwa kesi, Waziri limemgusa na kalizungumzia pia Hili la kubambika watu kesi tunaweza kuliondoa hata leo, kikubwa ni kuwa na nidhamu, inakuwaje unambambika mtu kesi ili akuletee pesa? Hiki ni kitendo cha rushwa na tuliangalie kwa pamoja na tutaliongea kwa undani Ijumaa

Hapa nimekusogezea pia baadhi ya picha za Waziri Kitwanga katika ziara yake.

????????????????????????????????????

Waziri Kitwanga (katikati) akitoka kuikagua moja ya nyumba ya zamani ya Jeshi ya Polisi ambayo inakaliwa na baadhi ya askari iliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar.

????????????????????????????????????

Waziri Kitwanga (kulia), Kamanda Suleiman Kova na kushoto ni  mkazi wa nyumba hiyo, ambaye ni askari Polisi, Nelson Chale.

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

Waziri Kitwanga akilikagua moja ya darasa linalotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Polisi Dar es salaam

????????????????????????????????????

Waziri Kitwanga (kushoto) akionyeshwa moja ya gari la maji washa, na Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova katika Kambi ya Jeshi la Polisi iliyopo Barabara ya Kilwa.

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

Waziri Charles Kitwanga  akizungumza na  waandishi wa habari

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana naMillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments