Duniani

Mfahamu aliyegundua PIN Code za ATM duniani, fedha aliyolipwa haifiki hata laki moja

on

James Goodfellow aiishiye Glasgow, Scotland miaka ya 1960 alikuwa ameajiriwa na kampuni ya Kelvin Hughes na kuagizwa ajaribu kuibuka na mbinu ya kulinda fedha kwenye ATM za benki ya Midland Bank ambazo kwa sasa ni HSBC.

Wazo lilimjia alipokuwa akitazama kadi iliyokuwa na data iliyoandikwa kwa program ya computer ambayo inaweza kusomwa na wanataaaluma wa computerAlitafakari kwa kina na kugundua kwamba ni mashine pekee iliyokuwa na uwezo wa kusoma namba hizo na kuzirejesha hadi mfumo wa namba za kawaida.

Kisha baadaye alitengeneza njia ya kusaidia watu kuandika namba ya siri ya kadi (PIN) kwa kutumia kadi ya plastiki yenye majina na namba ya account ya mteja ambazo zingeweza kusomeka kwenye ATM za benki hiyo ya Midland.

Lakini Goodfellow anasema hakulipwa pesa zozote zaidi ya dola kutokana na uvumbuzi wake kwa sababu aliambiwa ubunifu wake ulizingatiwa kwenye mshahara wake kipindi hicho.

>>>“Hata kama sikulipwa lolote lile sina kinyongo. Nimeridhika na kile nilichonacho, wazo la kuwa milionea wala halijawahi kunipita akilini.

Kiasi cha pesa anachosema alipokea ni dola 15 pekee ikiwa ni malipo ya dola moja kutoka kwa mataifa 15 yaliyoridhishwa na uvumbuzi huo na akayaomba yamlipe dola moja. Kwa sasa, kuna shughuli zaidi ya bilioni moja ambazo hufanyika kila siku zikitumia PIN.

Source:- DailyMail Online, Swahili Hub

James Goodfellow is the inventor of personal identification number technology (Family handout/PA)

James Goodfellow

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

ULIIKOSA HII EXCLUSIVE YA NISHA KUHUSU MAISHA, KAZI NA MAPENZI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments