Michezo

Wachezaji 6 wenye tuzo ya mchezaji bora wa Dunia lakini hawakutwaa Kombe Ligi ya Mabingwa Ulaya

on

Kitu muhimu katika maisha ya wanasoka wakubwa duniani sio tu kupata na kulipwa mshahara mkubwa, bali mataji ni miongoni mwa vitu ambavyo wachezaji wanavipa kipaumbele, March 2 nimekutana na list ya majina ya wachezaji sita mahiri kutoka sokka.com waliowahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia, lakini wameshindwa kutwaa taji la UEFA.

6- Michael Owen ni mchezaji wa mwisho wa Uingereza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or mwaka 2001, jamaa amewahi kushinda mataji kadhaa, lakini ameshindwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kuwa na mafanikio.

michael_owen_ballon_d_or_liverpool_photo-1024x694

Michael Owen

5- Pavel Nedved ni moja kati ya wachezaji waliowahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia akiwa na umri wa miaka 19 na klabu yake ya Lazio, Pavel pia anatajwa kama mchezaji mwenye mafanikio kutokea Czezh, lakini hakuwahi kutwaa taji la UEFA.

Czech Juventus midfielder Pavel Nedved holds the Ballon d'Or 22 December 2003 in Paris after being named the 2003 European Footballer of the Year. The prize, know as the Ballon d'or in French (the Golden Ball) and handed out by bi-weekly France-Football magazine, was awarded after a poll among journalists from the 52 countries affiliated to European football's governing body UEFA. MAFA PHOTO MICHAL SVACEK

Pavel Nedved

4- Fabio Cannavaro ni beki wa kati wa Italia na amewahi kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa na timu yake ya taifa ya Italia, licha ya kuwa alitamba na vilabu vya Juventus, Real Madrid na Inter Milan hakufanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

fabio-cannavaro

Fabio Cannavaro

3- Lothar Matthaus aliiongoza Ujerumani Magharibi kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1990, mwana unaofuatia Lothar aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ujerumani kutwaa tuzo ya Ballon d’Or na ndio mchezaji pekee wa Ujerumani kuwahi kutwaa tuzo hiyo.

Lothar-Matthäus

Lothar Matthaus

2- Ronaldo ametamba na vilabu vingi kwa mafanikio barani ikiwemo FC Barcelona na Inter Milan, Ronaldo amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mara tatu pamoja na Kombe la Dunia lakini hakuwahi kutwaa taji la UEFA.

Ronaldo-23

Ronaldo

1- Robert Baggio huyu huwa anapewa heshima ya kama mmoja kati ya wachezaji bowa wa muda wote kuwahi kutokea, amewahi kutwaa mataji mawili ya Ligi, Copa Italia pamoja na UEFA lakini hakuwa sehemu ya timu iliyosaidia kutwaa taji hilo.

roberto-baggio-milan-1456299401-800

Robert Baggio

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments