Hii inakuwa mara ya pili kukutana na taarifa ya ziara ya ghafla iliyofanywa na Waziri Mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa… mara ya kwanza ilikuwa siku chache zilizopita ambapo aligundua upotevu wa makontena 349, watu 12 wakakamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi.
Kituo cha ITV kimeripoti kuwa Waziri Mkuu huyo amefanya tena ziara ya ghafla bandarini Dar pamoja na Shirika la Reli TRL na kubaini ubadhirifu mwingine, ya leo inahusu upotevu wa makontena mengine 2431 !!
Naifatilia hii kwa ukaribu, chochote kitakachonifikia nitakufikishia wakati wowote !!
#Habari:Ziara nyingine ya kushtukiza ya waziri mkuu Mh.Majaliwa Kassim katika bandari ya DSM na TRL yabaini upotevu wa makontena 2431.
— ITV (@ITVTANZANIA) December 3, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.