Kwenye countdown zenye headlines za siasa bado macho na masikio ya wengi yako kwenye maeneo machache sasa hivi, nani atateuliwa na Rais kuwa waziri mkuu Tanzania? nani spika wa Bunge TZ? inawezekana waziri mkuu akateuliwa toka chama cha upinzani?
Nimempata kwenye exclusive Dk.Tulia Ackson ambaye ni wakili wa serikali ambaye pia aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali kwenye utawala wa Jakaya Kikwete, anayo majibu haya kuhusu uwezekano wa serikali ya Tanzania kuongozwa na Waziri Mkuu ambaye anatoka chama cha upinzani >>> ‘Sheria inamwezesha kufanya hivyo lakini Katiba imeweka Masharti kwamba Waziri Mkuu atoke wapi, hayo masharti yako matatu.
- Ni lazima Waziri Mkuu atoke katika Wabunge wa kuchaguliwa kutoka Majimboni.
- Ni lazima atoke chama chenye Wabunge wengi Bungeni, maana yake ni kwamba Rais akimteua Waziri Mkuu kutoka chama chenye Wabunge wengi ni lazima ataungwa mkono… lazima Waziri Mkuu aungwe mkono na Wabunge wengi.
- Ikitokea hakuna chama chenye Wabunge wengi Bungeni, Rais anaruhusiwa kuteua mtu yoyote ambaye ni Mbunge toka Bungeni.. awe ni Mbunge anayeungwa mkono na Wabunge wengi‘ >>> Dk.Tulia Ackson
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE