Kwa mujibu wa matokeo ya kidato cha pili 2016, kati ya shule 10 za sekondari zilizofanya vibaya kwenye mtihani huo, tisa zinatoka katika Mkoa wa Mtwara na moja Tanga. Shule za Mtwara zilizofanya vibaya ni Chingungwe, Malocho, Naputa, Chanikanguo, Mtiniko, Michiga, Msimbati, Salama na Lukodoka huku ya Tanga ikiwa ni Nywelo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo ya Mpanda kwa ajili ya kufungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda ameagiza uchunguzi ufanyike kujua sababu za kufeli wanafunzi kidato cha pili.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi Wizara wa Elimu Sayansi na Telnolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda mkoani Mtwara kufanya uchunguzi ili kubaini sababu zilizosababisha shule tisa za mwisho katika matokeo ya kidato cha pili kutoka mkoani humo.
Aidha ameziagiza halmashauri nchini kushirikiana na Idara ya Ukaguzi ili kuhakikisha wanawasimamia vizuri walimu jambo litakalowezesha kuboresha ufundishaji na hatimaye kupata matokeo mazuri.
VIDEO: Walichokisema CCM kuhusu madai ya baa la njaa nchini, Bonyeza play hapa chini