Habari za Mastaa

“Kalapina hana experience kubwa ila anajitaidi kuyajua madawa” Chid Benz

on

Msanii wa Bongofleva Chid Benz jioni ya April 28 2017 kupitia kipindi cha Clouds E kinachoruka kupitia Clouds Tv amefunguka mambo wakadha kuhusiana na mkali Kalapina ambaye hivi karibuni amekuwa anaharakati za kuwasaidia vijana kuacha dawa za kulevya.

Chid Benz amezungumza mengi hata kugusia swala lake la yeye kuwa rehabu kwa miezi mitatu kitu ambacho amekiri kuwa hakuwai kukaa kwa mda mrefu rehabu kama alivyokaa saivi katika rehabu ya Iringa na Tanga na kuwa kwa sasa yupo freshi.

.>>>”Nimejifunza vitu na naendelea kujifunza vitu vingi na kwasasa nimekaa muda mrefu zaidi maana sijawai kukaa rihabu miezi mitatu na ndomana unaona nimetulia mpka sahivi na nina miezi miwwili toka nimetoka niko poa niko freshi” – Chid Benzi

Pamoja na hilo Chid Benz hakusita kulizungumzia swala la kalapina kudai kuwa Chid Benz hajaamua kuacha dawa zakulevya na akiamua atacha hizo dawa za kulevya…>>>

“Kalapina unajua anazungumza ila hana experience kubwa sana ya dawa za kulevya ila anajitaidi kujua ishu za dawa ya kulevya lakini sisi amabo tupo kwenye dawa ndo tunaelewa kuwa nini kinatupeleka mpaka tunaingia kwenye dawa za kulevya nikitu ambacho ukikizungumza watu hawawezi kukuelewa na sisi ndotunaoishi maisha haya yeye hawezi kuelewa”

“Nihali ngumu sana ambayo inatukabili  japo tunapigana nayo kwaiyo na mimi watu wanatakiwa kunipongeza kwasababu kila siku naonesha nia yakupigana nayo” – Chid Benzi

VIDEO: “Nilikuwa natamani kupata mume ambaye atanijali na kuniheshimu” – Madam Flora

 

Soma na hizi

Tupia Comments